Faida za msanii kujiunga Basata

tizneez

Faida za msanii kujiunga Basata

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ni Shirika la umma lililoundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 23 ya Mwaka 1984.Historia inaonyesha kuwa, Sheria ya kuunda upya Baraza hili ilifanywa kwa kuunganishwa Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa ya Mwaka 1974 na Baraza la Muziki la Taifa (BAMUTA) ya Mwaka 1974. Baraza liliundwa ili lisimamie maendeleo ya sanaa nchini

Mapema mwaka huu kumekuwa na kuelemishwa zaidi wasanii wa kazi mbalimbali za sanaa kwenda kujisajili Basata ili kutambulika kisheria zaidi.

Msemaji wa Basata Ndugu Aristedes Basabya hakusita kuweka wazi faida za msanii kujiunga/kujisajili Baraza la Sanaa Tanzania. Ambapo aliiambia team tizneez “Faida za usajili ni nyingi lakini kubwa kuliko yote ni sheria inataka msanii asajiliwe, pia msanii kujisajili anaweka ulinzi wake katika kazi yake ili kazi yako isiibiwe na ulinde lazima usajili kazi yako.

Tatu msanii anaweza kuwa na safari zake kwenda nje ya nchi, hivyo usajili wako utakusaidia kwenda kutambulika kirahisi katika balozi zote. Pia kuna fursa ya matamasha ambayo huwa tunaletewa kutoka nje ya nchi au ndani ya wasanii kufanya maonesha hayo. Mfano kuna maaonesho kutoka Misri huwa ni kila mwaka. Na niwazi tamasha hili sisi tunatoa nafasi kwa wasanii ambao wamejisajili Basata tu.

Ni ngumu kutoa nafasi kwa msanii ambaye hajajisajili Basata.Hivyo kama hujasajiliwa ni wazi unakuwa upo nje ya uringo na hivyo utajikuta ukilaumu mambo mengi mazuri.”

Pia msemaji wa Basata hakusita kuweka wazi idadi ya wasanii wa kizazi kipya kuendelea kukua katika swala zima la kujisajili, ambapo sasa imezidi kuimarika siku baada ya siku.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez