Fahamu watanzania wanaofanya Bongo fleva/hiphop Hongkong

IMG-20160818-WA0102

De Junta ni kundi linaloundwa na wasanii wawili ambao ni Bobbo De Junta na King Saver De Junta, ambao uraia wao ni wa Tanzania. De junta ni kundi ambalo lilianzia Tabata posta, kutokana harakati za hapa na pale hatimaye wakali hawa wamehamishia shughuli zao za kimaisha Hongkong.

Mapema leo wakiongea na Team tizneez kwa njia ya simu wamesema “Tupo huku lakini tunajua thamani ya vipaji vyetu na Bongo Fleva/hiphop kwa ujumla, hivyo tuna kila sababu ya kuendeleza harakati za muziki kwa ujumla.

Na hivi karibuni tunatoa wimbo Mixtape yetu ya De Junta, ila sasa tumetanguliza wimbo mmoja unaoitwa Zamazabe. Video yake itakuja hivi karibuni so watu wajue tupo na tuna mipango mingi kuhusu muziki wetu”.

Sikiliza wimbo wao hapa chini.

Picha chini ya De junta Kutoka kulia ni King Saver na upande wa kulia ni Robby Runner.

IMG-20160818-WA0099

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez