Fahamu wasanii 5 bongo fleva/hiphop wanaohitaji management

images

Fahamu wasanii 5 bongo fleva/hiphop wanaohitaji management

Muziki wa bongo fleva/hiphop ni muziki uliotawala sasa katika ramani ya Africa. Lakini wasanii waliotawala si wengi kama vile inavyostahili kuwa.

Hakika muziki wa kizazi kipya umebalikiwa kuwa na wasanii wengi wenye vipaji vya hali ya juu.

Kuna wasanii watano ambao ni wazi kwa uwezo wao wangepata uongozi mzuri hakika tungewaona mbali zaidi ya pale ambapo tunawaona.

Mr blue, huyu ni moja kati ya wasanii watano ambao Team tizneez imetaka ufahamu. Hakuna anaeweza kupinga uwezo wa Mr blue ni uwezo wa juu, lakini msanii ambaye yuko kivyake zaidi katika kusukuma muziki wake. Lakini kama angepata uongozi wenye mipango mizuri hakika tungemuona mbali. Maana ni msanii mwenye uwezo wa kuchana na kuimba katika wakati mmoja.

Young Dee, ni msanii ambaye sasa amekuwa akizungumziwa zaid katika mitandao ya kijamii, lakini anazungumziwa katika mambo mabaya. Wengi wao wamekuwa wakishutumu kutumia madawa ya kulevya. Lakini ukija katika swala zima la kipaji ni msanii mwenye upekee katika ile aina yake ya kurap. Ni wazi Team tizneez haina mashaka na kipaji cha Young Dee.

Darasa, kama utanipenda ni wimbo wake unaofanya vyema sasa, tungo ni kitu pekee kinachomuweka tofauti na wasanii walio wengi. Darasa ni moja kati ya wasanii wa hiphop ambao wanajituma zaidi katika kuhakikisha muziki wake unafika mbali. Ila nguvu anayotumia kama angekuwa na uongozi mzuri hakika tungemuona mbali zaidi. Sikati tama ni wimbo wake ambao unaoaminika ni moja katia ya nyimbo chache za bora za hiphop zilitoka kuanzia mwaka 2012.

Nikki Mbishi,ni msanii anaeongoza kutoa nyimbo katika mtandao, ni wazi pia ni moja kati ya wasanii wachache wenye nyimbo nyingi. Huwezi kuacha kusema Nikk Mbishi ni msanii bora wa hiphop, lakini katika mfumo wetu wa ukanda,fitna na chuki ni wazi wenye tuzo za hiphop bongo hawafikii uwezo wa msanii Nikk mbishi. Ila kama pia angekuwa na uongozi ni wazi tungeona mazuri zaidi katika muziki wake.

Young Killer, kipaji chake na ufanyaji wa muziki wake ni tofauti kabisa na umri wake. Dear gambe ni wimbo wake ambao ulimtambulisha katika ramani ya Muziki wa kizazi kipya. Young killer kwa sasa hana uongozi unaoeleweka hii ni baada ya kutoka katika uongozi wa Classic Sound chini ya Mona Ganster, hivyo sasa ni mwenye kuyumba katika ramani ya muziki. Ni wazi ametoa wimbo mzuri na Mr blue ila ni ukweli usiopingika wimbo huo haupewi nafasi stahili katika vituo vya radio na runinga, lakini sijui ni kwanini maana ni wimbo mzuri. Ila hapa linapokuja swala la uongozi hakika lingesimamia hili la nyimbo kwenda zaidi katika vituo hivi.

Team tizneez imekuletea wasanii watano ambao ni wazi vipaji vyao ni vikubwa ila kukosa uongozi kunafanya kuyumba kwa kiasi fulani.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez