Fahamu vipengele 10 EATV Awards.

awards.png

Fahamu vipengele 10 EATV Awards.

Mapema leo hii kituo cha runinga EATV wametaja vipengele 10 ambavyo vitakuwepo katika tuzo zao ambazo zitaanza Desemba mwaka huu.

Vipengele hivyo ni

 1. Mwanamuziki bora wa kiume
  Mwanamuziki bora wa kike
  3. Mwanamuziki bora chipukizi
  4. Kundi bora la muziki
  5. Video bora ya muziki
  6. Wimbo bora wa mwaka
  7. Muigizaji bora wa kiume
  8. Muigizaji bora wa kike
  9. Filamu bora ya mwaka
  10. Tuzo ya heshima itakayotolewa kwa mtu au kampuni iliyochangia kwa kiasi kikubwa katika kazi za muziki.

Lakini kazi za sanaa zitakazoruhusiwa kuingia kwenye vipengele ni zile zilizotoka kuanzia Julai 1 2015 – 30 Juni 2016. Tofauti na tuzo zingine, wasanii wanaotaka kushiriki watalazimika kujaza fomu za kutaka kutajwa kwenye tuzo na kuwasilisha kazi husika ambapo mchakato wa uchambuzi wa kazi hizo utachukua kipindi cha mwezi mmoja kabla ya majina yaliyoingia kwenye tuzo hizo kutajwa na kuanza kupigiwa kura.

Hata hivyo pamoja na wananchi kupiga kura, kutakuwepo na jopo la majaji litakaloshiriki kupata washindi. Tuzo hizo zinazodhaminiwa na kampuni ya Vodacom, zitatolewa December 10 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

 

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez