FAHAMU PLAYLIST YA NYIMBO 5 ZA DOGO JANJA

SSSSSSSSSSS

FAHAMU PLAYLIST YA NYIMBO 5 ZA DOGO JANJA

My life ni wimbo wake unaofanya vyema katika vituo mbalimbali vya radio hapa nchini. Dogo Janja ambaye alijipatia umaarufu mkubwa katika wimbo wake wa kwanza unaoitwa Anajua ambao alimshirikisha Tunda Man.

Dogo hakusita kutaja nyimbo zake 5 ambazo yeye anaamini ni bora wakati wote,Anajua ni wimbo wake wa kwanza kuchagua/kuutaja ambao anaamini ni bora maana ndio wimbo uliomtambulisha kwenye ramani ya muziki wa kizazi kipya.

Yote ni maisha ya Madee ni wimbo uliofuata, ambapo alisema wimbo huu umeeleza mengi ambayo yanagusa maisha ya vijana walio wengi. Nakupenda hiphop ya Roho 7 ni chaguo lake la tatu ambalo ni wazi alisema”sijawahi hata kumuona huyu jamaa ila wimbo huu ni wimbo wangu ambao mara nyingi huwa nausikiliza.”

Jina langu ya Prof Jay ni chaguo langu jingine ambapo niliwahi kutamani pia jina langu liwe linavum kwenye yani kila nipitapo watu wajue mimi ni nani zaidi. Wimbo wangu wa mwisho ni wimbo wangu mwenyewe My life ambapo kabla ya kutoa wimbo huu nilikaa kimya kwa muda wa miaka mitatu na nusu bila kuimba chochote, na mengi yametokea hapo katikati”.

Dogo Janja alisema hayo na kuchagua nyimbo hizo katika kipindi cha Playlist cha Times Fm kinaongozwa na LilOmmy au Omary Tambwe.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez