Fahamu nyimbo mbili zilizopotezwa na kiki.

Fahamu nyimbo mbili zilizopotezwa na kiki.

Neno kiki limeibuka miaka kadhaa nyuma ni katika miaka ya 2013 lakini 2016-2017 kiki imechukua nafasi kubwa katika muziki wa kizazi kipya.

Katika uhalisia kiki zimeharibu mno muziki, lakini pia kiki imeharibu heshima za wasanii wengi tu.
Licha ya wengi kuamini kuwa mafanikio huletwa kwa kiki na hata kudhani kwenda kimataifa ni kufanya jambo baya ambalo litazungumziwa zaidi katika mitando ya kijamii lakini pia katika vyombo vya habari.
Nguvu ya kiki imefanya wasanii kukosa ubunifu katika kazi zao bali kuegemea katika mlengo wa kiki na huku wakiamini ule msemo wa Fid Q wa “umaarufu hauji bila skendo” ila wapo ambao wameishi nje neno hilo akiwemo yeye mwenyewe Fid Q.
Kwanza jamii inapaswa kujua kua ukweli hauna baba wala mama ukweli utabaki kua ukweli wakati wote bila kujali nani ni nani.

Lakini ukweli utatuweka huru na kubadilisha fikra potofu za wasanii na mashabiki ambao akili na mwili zimelala katika kiki.
Bila kiki muziki unaweza kufanyika vyema tena katika kiwango cha juu na heshima zaidi.
Team tizneez tumetazama nyimbo mbili tu ambazo nguvu ya kiki ilizidi wimbo husika, ilihali zipo nyimbo nyingi zilizopoteza maisha kwaajili ya kiki tu.

Wimbo wa kwanza ni wimbo wa Ommy Dimpoz ambao uliitwa Wanjera. Huu ni wimbo mzuri ambao ulikuwa na sifa zote za kuwa wimbo mkubwa katika mitaa na vilinge vya wapenda muziki wa kizazi kipya. Ila kiki ya kutoka kwa picha za Ommy Dimpoz akiwa na Wema Sepetu katika mapozi ya sio na maana mbele ya jamii hakika ilichangia kuupoteza wimbo huu. Ni wazi jamii ilizungumza zaidi kuhusu picha hizo na hata wimbo ulivyotoka haukua na nguvu bali watu walibaki katika nguvu ya mabishano juu ya Wema kua na mahusiano na Ommy lakini kuwaza mbona Ommy na Diamond Platnumz ni marafiki kwa wakati huo.
Bila watu kujua picha zile zilipigwa wakati wa utengenezaji video Afrika ya kusini. Kimsingi haikua na sababu ya msingi kuvujisha picha na Ommy kujifanya ni mpenzi wa Wema Sepetu. Lakini msisahau msemo usemao “Huwezi kuona msitu ukiwa msituni”
Wimbo mwingine ambao umepotezwa kwa ukubwa wa kiki ni wimbo wa Ben Paul. Ni wazi katika utafiti mdogo zaidi tuliofanya watu wengi hawajui hata jina la wimbo ila wanajua tu Ben Paul amepiga picha za utupu.
Wimbo huo hauna maisha ya kufanya vyema katika uwanja wa muziki wa kizazi kipya.

Bali Ben Paul kubaki na aibu yake ambayo ameishusha kirahisi mfano wa mtu afunguapo taulo bafuni
Kiki ya kupiga picha za utupu na wimbo ni wazi vimepishana mbali mno. Lakini aina ya muziki aliotoa ni sauti mpya masikioni mwa watanzania hivyo hakupaswa kutumia kiki ambayo ametumia.

Lakini jamii yapasa ijue “Hakuna shule ya akili”

Ila hatujui mshauri wake ni nani ila yapasa wasanii wajue kiki haina maana kwa maana inaweza ikakuzidi maana na ikaharibu maana yenye maana katika wimbo wako.

Tuachie Maoni yako hapa.
Follow us
Twitter Tizneez
Facebook Tizneez
InstagramTizneez
Youtube Tizneez