Fahamu kuhusu Swahili hip hop band

255653118413

Swahili Hip Hop Band (SWAHIBA)
Hii ni bendi ya muziki wa hip hop wenye vionjo vya asili vya tamaduni kadhaa za Kiafrika (Traditional hip hop music).  Muziki huu sisi ni wa kwanza kuufanya tumeupatia jina la “Tubite fleva”. Tubite ni neno la kihehe linalomaanisha Twende. Muziki huu unahusisha midundo yenye vionjo vya asili na matumizi ya lugha za makabila mbalimbali ya Africa. Muziki unahusisha live performance na biashara ya bidhaa za asili. Nyimbo tulizofanya  ni “AFRICA TUBITE” ambayo video yake inapatikana Youtube na mpya inayotarajiwa kutoka wiki ijayo inaitwa “SWAHILI” zikiwa ni nyimbo za utangulizi wa Album. Bendi ilianzishwa mwaka 2014 na makazi yake ni Dar es Salaam, Tanzania.