Exclusive!”Nilimsaidia Lord Eyez sikuwa nimemsaini, Vitu vingine kwasasa ni juu yake mwenyewe” Baraka Da Prince.

Exclusive!”Nilimsaidia Lord Eyez sikuwa nimemsaini, Vitu vingine kwasasa ni juu yake mwenyewe” Baraka Da Prince.

Sikiliza Sauti hapa chini. Baraka Akizungumza na Team Tizneez

Exclusive!”Nilimsaidia Lord Eyez sikuwa nimemsaini, Vitu vingine kwasasa ni juu yake mwenyewe” Baraka Da Prince.

Huu chini ni uhalisia mdogo kati ya mengi.

Kipi kipo kati ya Baraka Da Prince na Lord Eyez? Maana nguvu ya kusemwa na wapiga miluzi hodari kama alimsaini ilikuwa kubwa. Licha ya katika mahojiano mengi ambayo alikuwa anafanya Baraka alikuwa akiweka wazi kuwa yupo kikazi na amemsaini Lord Eyez.

Mapema akizungumza na Team Tizneez aliweka wazi kuhusu uwazi uliopo kati yake na Lord Eyez ambaye ni moja kati ya wasanii waliokuwa wanaunda kundi la Nako 2 Nako pamoja na kuwa kati ya wale watano wanaounda kampuni ya Weusi.

Jambo la Baraka kumsaini Lord Eyez ilikuwa ni habari njema kwa wapenzi na mashabiki wa Lord Eyez, lakini pia hata Joh Makin hakusita kuweka wazi hisia zake pale ambapo aliulizwa juu ya Baraka kumsaini Lord Eyez ambapo Joh alijibu “Ni jambo zuri na hakuna ubaya kati yangu au kati weusi na Lord Eyez”

Leo hii Baraka anapopindua maneno kuwa hakuwahi kumsaini Lord Eyez ilihali mwanzoni alitamka na wasanii wengi walitoa maono yao juu ya jambo hilo, je! leo hii nini kimetokea? Ila wapo ambao husema Lord Eyez si msanii mwenye nidhamu ya kazi wakati wote, je nidhamu huenda ikawa chanzo? Licha ya Baraka kukataa kabisa kuweka wazi juu ya jambo hilo Zaidi ya kusema mkataba ni jambo lenye kifungo hivyo hakutaka kuwa kifungoni kati yake na Lord Eyez.

Je!Lord Eyez ataweza kusimama pekee yake kwa sasa? Maneno yasiyo na vitendo juu ya kurudi kwa kundi la Nako 2 Nako ni mengi, ila pia Lord Eyez aliwahi kuiambia Team tiznez mwaka huu kuwa “Kwasasa nipo mimi kama mimi na nipo na project zangu Zaidi”

Je! Weusi watamrudisha kundini Lord Eyez katika muda huu?

Tuachie maoni yako hapa

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Attachment