DUDU BAYA ATOA KAULI YAKE KWA SHETTA

Dudu-Baya

Dudu baya ambaye ni miongoni mwa wasanii waliochagia kukua kwa bongo fleva/hiphop ndani na nje ya nchi.Dudu baya ambaye pia ndiye msanii wa pili kufuata kati ya wasanii wenye album nyingi, akiwa na album 5 wakati nafasi ya kwanza ikiongozwa na Mr II Sugu akiwa na album 10.

Ni miezi kadhaa tangu wasanii waanze kujipa majina ya wanyama, licha ya majina hayo kuonekana kuleta kutokuelewana baina yao. Mr Blue ni moja kati ya msanii aliyepishana kauli na Diamond pale msanii Diamond alipojiita Simba, lakini pia msanii  Afande Selle ni msanii aliyejiita simba kwa miaka  mingi licha ya kutokuongea chochote baada ya Diamond na Mr blue kugombea jina hilo.

Shetta nae ni msanii mwingine aliyejibatiza jina la mnyama na kujiita Mamba. Mapema leo Msanii mkongwe Dudu Baya ameibuka na kusema “Shetta aache kutumia jina hilo maana hafanani nal, pia ana niharibia sifa yangu”

Picha ya shetta chini

Shetta_lg_lrg

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez

 

 

 

Source Planet Bongo Earadio