Dogo Janja ni vyema kuheshimu mahojiano

Dogo Janja ni vyema kuheshimu mahojiano

Mpendwa msanii Dogo Janja ni vyema kuheshimu mahojiano hata kwa ngazi ya mtandao.

Lakini “utumwa mbaya ni kufikiri yakuwa mawingu ni mahala salama ilihali ni mahala pasipo na makazi ya kudumu”
Ni jambo baya kupewa mahojiano iwe kwa simu au uso kwa uso na kushindwa kutoa ushirikiano yaweza kuwa umfahamu huyo mtu lakini yapasa umsikilize.

Ni vyema kujifunza kusema “Samahani muda huu sipo tayari kwa mahojiano” lakini si kujibu majibu ambayo yatamfanya mhusika aliyekutafuta kuhisi hana uthamani.(Ushirikiano)

Jambo baya ni kukaa kimya na kuwekea vinyongo ambavyo kimsingi havina maana bali yafaa ukweli uweke wazi kwa maana ya kumjenga msanii.

Tuipende kweli maana kweli utatufanya tuwe huru lakini tuwe na upendo. Kwa maana nyakati zote yafaa mjue yakuwa “Msema kweli hana wajoli”

Ni vyema Dogo Janja ujirekebishe katika hili maana nyakati hubadilika.

Lakini huenda hatupaswi kuyasema haya juu yako maana waswahili husema “Usimlaum mkwezi nazi imeliwa na mwezi” (Akili)

Ila yapasa ufahamu “Mdharau biu, hubiduka yeye”

Ni muda mwema wa kutafakari umuhimu wa mahojiano katika ngazi zote lakini kwa mtu yoyote wa Media haijalishi anatokea upande gani. (Nidhamu)

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa