DOGO JANJA ANASTAHILI PONGEZI

SSSSSSSSSSS

KItambo mimi nachana zaidi ya wanyamwezi nyie moyoung hamniwezi mtapenga sana mpaka totoro” la la le le am living my life, hii ni baadhi ya mistari inayoptaikana katika wimbo wake mpya ulitoka wiki iliyopita siku ya alhamisi. “My life”

Wimbo huu umetoka baada ya kimya cha miaka mitatu na nusu, ambapo hapo kati katika maisha ya muziki ya Dogo Janja yalitokea mengi, hakika hakuna anayefuatilia kwa ukaribu muziki wa kizazi kipya asiyejua yaliyotokea. Binafsi katika mambo ambayo yalinifurahisha ni ule uamuzi wake wa kuamua kurudi Tip Top Connection.

Tip Top Connection ni miongoni mwa uongozi mkubwa hapa nchini, ambayo imeshika mastaa wa bongo fleva kama Madee, Tunda Man,Dogo Janja na wengine wengi.

Muziki wa kizazi kipya umeshatoa wasanii wengi ambao walifahamika Afrika Mashariki, lakini mwisho wa walio wengi waliopotea na tusijue kile wanachokifanya. Wengi wao hupotea kwa kukosa uongozi wa kuwaongoza katika kazi zao za kimuziki, na hata wakisema wanarudi kwenye game hushindwa maana hutoa nyimbo ambazo hazifanani na hadhi yao ambayo waliiijenga mwanzo.

Wengi hawakutarajia ujio huu wa Dogo Janja, amebadilika vingi kuanzia staili yake ya kuchana ambapo ameonekana ametulia na kunata na biti, kuimba kidogo, hakika amejua kwenda sambamba zaidi na biti, kwa kawaida tu ukisikiliza utajikuta ukitikisa kichwa.

Kwa umri wake Dogo Janja kama ataongeza na Nidhamu ya kazi yake ya kimuziki hakika atafika mbali kimuziki.

Ni vyema kujenga tabia ya kupongezana pale mtu anafanya vyema katika kile akifanyacho, team tizneez inakupongeza kwa kazi yako ya my life.

Nidhamu!Nidhamu!Nidhamu!kitu unachopaswa kukipa kipaumbile kwa kile unachokifanya kila iitwapo leo ili kupata mafanikio katika maisha yako.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez