Dogo Awaandikia ujumbe wasanii wenzake juu ya tukio la Nandy

Dogo Awaandikia ujumbe wasanii wenzake juu ya tukio la Nandy,

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Dogo Janja hakusita kuweka wazi ujumbe wake kwa wasanii wenzake baada ya tukio la kusambaa kwa video ya faragha ya Nandy na Billnass.

Kupitia mtandao wa picha ‘Instagram’ Dogo Janja ameandika “Nahisi nnaweza kumaindiwa Leo na wasanii wenzangu ila lazima MTU aanze ndo hili donda ndugu litapona.

Wasanii sisi ni masnichi sana aise, baada ya hii ishu ya nandy ndo nimepata uhakika.

Wakati wa ishu ya Roma nilianza kuliona jinsi kwenye makundi pembeni watu kibao walikuwa wanafurahi tena maneno kibao kama atakoma, amezoea huyo.

Jana na juzi nimekaa na watu wasanii wakubwa tu na wote walikuwa wanasema bora limemtokea nandy hili angalau spidi za show zitapungua.

Bora basata ingemfungia miezi 6 apotee kidogo, walikuwa wanapiga story kama utani ila moyoni nimefikiria sana.

Wasanii tuache roho mbaya, wote sisi maskini tunahangaikia ugali.

Tukipata ajali kazini, tusiombeane mabaya tutafute amani. Vita iwe kwenye kazi jamani. Hizi story za kufurahi ajali kazi mi nazikataa”

Mwisho

#TuzungumzeMuziki