DIAMOND PLATNUMZ NA VANESSA MDEE WANG’ARA NIGERIA

photo-collage-2
Tuzo za Afrima zimetolewa jumapili ya jana katika jiji la Lagos Nigeria ambazo zilihusisha wasanii wanne kutoka hapa nyumbani Tanzania.Diamond,Lina,Vanessa pamoja na Ally Kiba ndio wasanii waliotuwakilsha katika tuzo hizi za Afrima.
Katika tuzo hizo msanii Diamond Platnumz amezidi kushangaza walio wengi baada ya kuchukua tuzo 3,ambazo moja ni Msanii bora wa mwaka ambapo hapa alikuwa akichuana na mkali,Wizkid,Davido.Ally Kiba,Jose Chameloone,Yemi Alade,Sarkodie na Mr flavour.
Vipengele vingine alivyoweza kushinda ni Best song of the year na kile kipengele cha Best male eastern of the year.
Capture
Hata hivyo mwanadada (Vee Money)nae ameendeleza kuonyesha ukubwa wake katika muziki wake baada ya kuibuka mshindi katika kipengele cha Best african pop kupitia ngoma yake ya hawajui.
Team tizneez inawapongeza kwa ushindi huu ni wazi mbongo fleva inazidi kupata thamani kubwa ndani ya africa na nje pia.
1490702_721529807859749_1396179348_o