Diamond Platnumz na Ali Kiba wawakilisha vyema muziki wa kizazi kipya Uganda.

Diamond Platnumz na Ali Kiba wawakilisha vyema muziki wa kizazi kipya Uganda.

Diamond Platumz na Ali Kiba ni wasanii wazuri ambao tumebarikiwa kuwa nao katika ramani ya muziki wa kizazi kipya.

Licha ya ushindani wa kikazi ambao wamekuwa na nao sasa kwa miaka kadhaa hasa katika soko la ndani, lakini wasanii hawa wameendelea kuiwakilisha bongo fleva vyema katika anga mbalimbali.

Mapema usiku wa kuamkia leo Mkali na Ali Kiba na Diamond Platunum wameweza kuipeperusha vyema bendera ya muziki wa kizazi kipya nchini Uganda.

Katika tuzo za Hipipo ambazo zimetolewa Nchini Uganda Ali kiba ameweza kuibuka mshindi wa kipengele cha wimbo bora wa mwaka ambao ni ‘Aje” lakini Diamond akiibuka mshindi wa kipengele cha mwanamuziki aliyeweza kuwa juu katika muziki industry  kwa miaka 5 mfufulizo.

Team Tizneez tunawapongeza kwa ushindi huu.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa

Attachment