DIAMOND PLATNUMZ AUPONGEZA UPINZANI

D
Ikiwa ni saa chache tangu kutangazwa kwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli ambaye alikuwa ni mgombe wa Chama Cha Mapinduzi.
Daimond amekuwa n miongoni mwa wasanii waliandika kuhusu ushindi huo, Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeandika “Heri ya kuzaliwa na pongezi nyingi Dr.John Magufuli Pombe pamoja na uongozi mzima na wanachama wote wa CCM kwa kuweza kufanikisha kuingoza tena Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Lakini pia niwashukuru na kuwapongeza vyama vya upinzani kwani naamini amshaamsha mliofanya mwaka huuitasaidia kuongeza kasi za utendaji wa viongozi wetu pendwa, na nchi yetu kupata maendeleo zaidi.Hakika uchaguzi ulikuwa ni wakipekee.Ni muda wa watu wote kushirikiana kwa pamoja na kujenga nchi.Kumbuka hakuna atakae kuletea chumbani kwako amka uwajibike maana hata punda hajasoma lakini hakosi kazi.”Ameandika Diamond.