DIAMOND PLATNUMZ ATOA RUHUSA MEDIA KUCHEZA COVER YA WIMBO WAKE

howwe_1827a065db29075add542c95bd2c8cd0_1436369907

Utanipenda ni wimbo unaofanya vizuri nje kwenye media za ndani na nje ya nchi pia ,wimbo huu ni mali ya mkali Diamond Platnumz,uliofanywa na mtayarishaji Tuddy Thomas.

Tangu utoke wimbo huu msanii Diamond Platnumz alitoa ruhusa za msanii yoyote kurudia wimbo,na wengi wakaonekana kufurahishwa na kitendo hicho. Na mpaka sasa ni wasanii wengi wamejitokeza na kurudia wimbo huu wa utanipenda.

Mapema jana msanii Diamond kupitia mtandao wa Instagram aliandika “Support mnayozid kuipata juu ya ngoma yangu ya utanipenda ni kubwa sana.Wengi wameifanya hii nyimbo cover, Yani kuirudia kuimba kwa taaluma zao.Tafadhali radio na tv stations wanapozileta nyimbo hizo kwenye media zenu zikiwa zina viwango ni ruksa kuzicheza. Maana huwezijua cover ama nyimbo hizo zinaweza kumfikisha wapi kesho na kesho kutwa”

Mwisho

www.tizneez.com

instagram tizneez

twitter tizneez

facebook tizneez