DIAMOND PLATNUM ADAIWA KUTELEKEZA WATOTO,ASHINDWA KUWALIPIA ADA

11164584_1636778786559971_877490440463341046_n
Mwanamuziki nchini Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond’, anayejivunia kwa kujitangaza kimuziki ndani na nje ya nchi anadaiwa kutelekeza watoto aliojitolea kuwasomesha hali iliyopelekea watoto hao kushimamishwa masomo.
Inadaiwa kuwa watoto hao Hillary na Hamis, wamesimamishwa masomo tangu Aprili mwaka huu, jambo ambalo limeonesha kuwaumiza wazazi wao ambao walikuwa wanamatumaini kuwa watoto wao watafika mbali kimasomo.
Tukio lilikuwa hivi:
Watoto hao walishinda katika mashindano ya Ngololo Januari mwaka jana ambapo mwanamuziki huyo alijitolea kuwasomesha na kuwatoa katika shule za kawaida na kuwapeleka katika shule ya East Africa International iliyopo Mikocheni Jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mwalimu mkuu wa shule hiyo Mercy Githirua, amedai kuwa ni kweli amewasimamisha watoto hao masomo kutokana na kushindwa kulipiwa ada na kudai kuwa wamefanya hivyo kutokana na kuvumilia kwa muda mrefu.
Kwa upande wa wazazi wamesema kuwa wameumia sana kuona watoto wanakosa masomo na kudai kuwa wamemfuatilia sana mwanamuziki huyo bila mafanikio na kuongeza kuwa mameneja wa msanii huyo wamekuwa wakiwazungusha kwa madai mwanamuziki huyo yupo kwenye shoo
SOURCE Ben Kalonga.