Daz Baba Aeleza sababu za kuwa kimya pia akana kutumia madawa ya kulevya.

a8b37183237845fe540216666ea3e8e2

Daz Baba Aeleza sababu za kuwa kimya pia akana kutumia madawa ya kulevya.

Daz Nundaz ni kundi lake ambalo alikuwa nalo tangu akianza muziki kabla ya kutokea kutokuelewana na baadae kuanzisha kundi lake ambalo linaitwa Tanzaniano.

Wimbo kama nipe tano,wife, elimu dunia, na nyingine nyingi zilimpa umaarufu mkubwa ndani ya Tanzania na nje pia.

Akiongea na team tizneez Daz Baba hakusita kuweka wazi ukimya wake kwenye ramani ya muziki wa kizazi kipya, ambapo amesema “baadhi ya studio ambazo nakuwa nimerekodi huwa wanachelewa kumix nyimbo hivyo inafanya niwe kimya. Lakini sasa nimeshaamua kufanya kweli zaidi katika studio nyingine kubwa hivyo wakati wowote nakuja kwenye nafasi yangu.

Lakini pia swala la kutumia madawa ya kulevya hapana situmii. Wewe mwenyewe unaona hapa home palivyo mimi naishi na mama yangu baba alishafariki hivi kama ningekuwa natumia madawa je ningeweza kuwa mtunzaji wa hizi mali? Hivyo ni watu wachache tu wameamua tu kunichafua na sipati faida yoyote ile kwa kile ambacho wanakiandika kwenye magazeti yao.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez