Dayna Nyange Asema menejimenti anayoitaka

Dayna-nyange

Dayna Nyange Asema menejimenti anayoitaka

Angejua ni wimbo wake uliofanya vyema na kuzidi kumpa heshima, maana ni wazi ni msanii mmoja wapo wa kike mwenye kuonyesha nidhamu mbele ya mashabiki kuanzia katika mitandao ya kijamii mpaka kwenye maisha ya kawaida.

Dayna akiongea na team tizneez amesema “Namshukuru mungu kwa hapa nilipofika, maana nimefika hapa bila hata kuwa na menejimenti yoyote ile. Lakini ni wazi natamani kuwa na menejimenti, ila natamani kuwa na menejimenti ambayo inajua muziki vizuri. Pia iwe inajua changamoto za watoto wa kike, awe na uelewa wa muziki tufanye kazi tufike mbali.

Kikubwa wengi wanafeli maana wanaamini kuwa na meneja lazima awe na hela ndio unakuwa umemaliza kila kitu ambayo unakuta mwisho wake wanaishia pabaya. Maana mnaweza kuwa na hela nyingi lakini msiwe na mipango, ila unapaswa kuwa na mtu mwenye kujua jinsi ya kuendesha muziki zaidi.”

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez