DARASA NA HOFU YA KUGAWA MASHABIKI

index
Haye heya ni wimbo wake msanii Darasa unaofanya vizuri akiwa meshirikiana na Mr Blue,Na wakati huu yuko katika hatua za mwisho kukamilisha video inayofanywa na Director Hanscana.
Akiongea na Team tizneez Darasa hakusita kuweka wazi sababu zilizomfanya kuto kushiriki katika kampeni za uchaguzi zilizomalizika hivi juzi.
Darasa alisema “Mimi ni msanii na nina mashabiki wengi wa kila rika,na kabla ya kufanya kitu ni lazima ufikirie.Sikuweza kushiriki katika kampeni kwani nilikuwa na hofu ya kugawa mashabiki wangu,mfano nina shabiki yupo CCM na mwingine CHADEMA sasa kama nitakuwa upande mmoja lazima mwingine nimpoteze.Sikutaka hayo ndio maana niliamua kukaa kimya”.Alisema

Instagram/TIZNEEZ
Twitter/TIZNEEZ
Facebook/TIZNIZ