“Daima nitazikumbuka Tuzo za Kili kwa sababu mbili tu”Fid Q

Hiphop Icon kutoka ardhi ya Tanzania Fid q ambaye ameendelea kubaki na heshima yake katika uwanja wa hiphop kwa kuendelea kubaki kwenye misingi licha ya wengi kubadilika.

Mapema leo katika mtandao wa ‘Twitter’ Fid Q hakusita kuandika kumbukumbu zake juu ya Tuzo za Kili Music ambazo mpaka sasa haieleweki hatma yake.

Fid Q ameandika Daima nitaikumbuka KILI kwasababu MBILI tu za msingi•• 1- ILIKUA INANIMWAGA SANA 2- KISHA IKANIBEBA 😂

Ama baada ya kuwaelezea furaha yangu,naomba nilete masikitiko niliyonayo pia••ni kwamba hadi hivi sasa hatujui kama KILI itarudi tena au 👎🏾

Siku kama ya leo.. mwaka 2014 ndio nilikwara zile KILI mbili•• 1- best hip hop artist 2- best lyricist

 

Kumbukumbu kwa hisani ya FB 🙏🏿

Mwisho.