Cyril Kamikaze Afuta jina la Ray Vany wa WCB katika wimbo wake

1b810ecb3e3d9762f0da9ee66c80ddf0

Kwa kile kilichotokea jana kati meneja wa Diamond Platnumz ndugu Sallam Sk kusema “Hakuna Collabo na Raymond, alimuomba Ray amuandikie na apewe melody siku nyingi sana! Hiyo nyimbo hatuuitambui”.

Na ni wazi Cyril Kamikaze alijibu kupitia mtandao wa picha ambapo alieleza jinsi alivyosikitishwa juu ya meneja wa Wcb kukana wimbo huo ambao ni wazi alifanya na Ray vany kabla ya kuwa chini ya label hiyo.

Mapema leo kupitia mtandao wa picha Cyril hakusita kuweka post aliyoandika “Ok nadhani issue ilikua ni kumtaja Ray kuwa nimemshirikisha na kiukweli ameshiriki kuandika huu wimbo asilimia 70 nzima na hata kuweka sauti zake na deal tukai kamilisha ,na kazi tumeifanya kabla Ray hajaenda label mpya kama nilivyo sema jana .. Basi jina nimelitoa CYRILL KAMIKAZE – CHEZA KIDOGO …. Bonyeza link kwenye BIO ku download huu wimbo .. #singidaboy”

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez