Coke Studio Africa maana ya halisi ya muziki mzuri.

Coke Studio Africa maana ya halisi ya muziki mzuri.

Waswahili husema “Shahidi ndiye mwenye neno” hivyo tuna kila sababu ya kuwa shahidi juu ya kusema “Coke Studio Africa maana ya halisi ya muziki mzuri”

Msimu wa tano wa Coke Studio Africa unaendelea na jumamosi ya tarehe 23.9.2017  tumeweza kuona muendelezo mzuri ambao kwa hakika umevutia kwa kila jicho la mtazamaji lakini sikio lilipata kusikia muziki mzuri tokea Coke Studio Africa.

Msimu huu wa tano na kipindi cha tatu Nandy wa Tanzania na Betty G kutoka Ethiopia walikutana kwa pamoja ili kutengeneza muziki mzuri na kila mmoja kugundua muziki wa kila mmoja wao.

Lakini wakati huo Kaligraph Jones ambaye ni mwana hiphop tokea Kenya alikutana na msanii wa Rnb Bluce Melody tokea nchini Rwanda na waliweza kufanya kazi pamoja.

Y Kibenda ambaye anawakilisha Uganda alipata wakati mzuri kufanya kazi na Mr Bow tokea msumbiji lakini Jay Prayzah tokea Zimbabwe alishiriki nao kwa pamoja.

Hakika Coke Studio Africa maana halisi ya muziki mzuri kwa maana ya wasanii wote kuweza kutoa burudani safi yenye ubora kwa wakati huu na ujao.

Kama hukupaswa kutazama shoo hii ni wazi tumekuwekea hapa chini Bonyeza linki kutazama.