CHRISTIAN BELLA, AMPA MBINU MPYA ALLY KIBA

Msanii anaefanya vizuri na nyimbo yake ya nani kama mama aliyomshirikisha Ommy Dimpoz,Christian Bella ambaye pia moja kati ya wasanii wanafanya vizuri zaidi katika muziki wa bongo fleva licha ya kuwa ni moja ya wasanii wanaounda Band ya Malaika yenye maskani yake Jijini Dar es Salaam.
Christian Bella Alisema “Ally KIba ni msanii mzuri sana katika wakati wote tangu nimfahamu,ana kila sababu ya kuwa msanii mzuri maana ana vocal,melody na kujua kuandika nyimbo kwa uzuri, ila anakosea vitu vichache tu.Moja ya vitu anavyokosea Ally Kiba ni kuwa kimya kwa kipindi flani tena kwa muda mrefu,sasa anachotakiwa kufanya mda huu ni kuachia nyimbo mara nyingi awezavyo yani bandika bandua nasema Ally KIba n msanii mkubwa tu.”
Bella alisema hayo katika kipindi cha Mboni Show kinachorushwa na kituo cha TBC,Baada ya Mboni kumuuliza wasanii anawakubali kwa hapa Tanzania,hata hivyo pia alimtaja msanii Diamond Plutnum kama moja ya wasanii wazuri huku akimzungumzia Belle 9 kuwa ni moja msanii mzuri wakati wote.
Mwisho.

 

TANGAZA NASI