Chid Benz Yupo sawa kweli?, au ndiyo mfa maji?

maxresdefault

Chid Benz Yupo sawa kweli?, au ndiyo mfa maji?

Ni wiki 1 tangu team tizneez kuandika makala ya Wimbo wa Joh Makini “Ufalme”ni jibu tosha kwa Chid Benz.

Makala hiyo ilikuja baada ya Chid Benz kuongea mambo ambayo hayakuwa mazuri juu ya Joh Makini lakini pia Nay wa Mitego.

Mapema leo kupitia kituo cha Ea Radio Chid Benz Hakusita kusema “Nukuu” “amewataka watu kutomuelewa vibaya alipowaongelea Joh Makini na Ney kwani wana uwezo mkubwa kisanii”

Hili limenifanya nione ni jinsi gani amekuwa kigegeu katika kauli zake. Lakini pia kauli zake zinanifanya nihoji Chid Benz yuko sawa? au ndio mfa maji haishi kutapatapa? Katika makala ya “Kurudi ghafla na kupotea ghafla” niligusia mengi katika kurudi kwake naona imekuwa haraka mno.

Pia ni vyema kuchunga kauli zake ajue huu ni muziki sio siasa. Muziki umebadilika mashabiki wanataka kazi nzuri na sio maneno maneno.

Naamini kwenye kipaji cha Chid Benz naamini kama atatulia atarudi kwenye nafasi ambayo aliwahi kushika maana muda bado anao.

 

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez