CHID BENZ SIPENDI KUSIKILIZA WIMBO WANGU

chidbenz

CHID BENZ SIPENDI KUSIKILIZA WIMBO WANGU

King kong, chuma, hizi ni baadhi ya a.k.a zake kati ya zile nyingi,Chid Benzino ambaye aliwahi kufanya vyema na ngoma kama Chaguo langu, Umenisoma, Nitabaki Nakulilia, pamoja na nyingine nyingi.

Lakini kati ya zote wimbo wa Dar stand up ni wimbo ambao una nguvu kubwa katika jamii, wimbo huu umekuwa ukiinua mashabiki katika kila show ambayo atafanya Chid Benz.

Chid ambaye sasa yuko mbioni kurud kwa kishindo katika game ya hiphop leo hakusita kuweka wazi hisia zake juu ya wimbo wake wa dar stand up. Chid Benz alisema “wimbo huu kwangu ni wimbo wa pekee ni nwimbo mkubwa sana leo hata uweke wasanii 30 waambe na kuimba tena lakini ikipigwa dar stand up lazima uone tofauti ya mashabiki ilivyo, hakika hakuna atakaye kaa. Hivyo sipendi kuusikiliza mara nyingi huwa nafanyaia show tu, maana wimbo huu huwa unaniingia sana katika hisia kiukweli unanikumbusha mbali.”

Hata hivyo chid benz alisema “hivi karibuni narudi tayari nimesharekodi na nimemshirikisha Mr blue mdogo wangu mwenyewe, watu wategeme makubwa mwaka huu.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez

 

 

 

 

 

Source Plannet Bongo Ea radio