“Chid Benz amekuja kumpokea shujaa” Nash Mc

“Chid Benz amekuja kumpokea shujaa” Nash Mc

Zima,Naandika,Mwanangu,Kaka suma,ni moja kati ya nyimbo chache zilizoweza kufanya vyema kwa mkongwe wa hiphop Nash Mc.

Nash Mc ambaye misimamo yake imeendelea kumpa heshima kubwa katika vijiwe vyote vya muziki wa hiphop.

Mapema leo kupitia mtandao wa Picha Instagram hakusita kueleza kukutana na Chid Bez ambaye ni moja kati ya marapa bora waliowahi kutokea kwenye ramani ya muziki wa kizazi kipya.

Nash ameandika “Dakika kadhaa zilizopita rafiki yangu wa siku nyingi kabla hatujakua na nafasi kubwa katika Sanaa leo tumekutana studio Kiri Records baada ya miaka kibao. Nilikua nasikiliza hatua za mwisho za wimbo wangu wa Shujaa mara Chuma huyo akaingia,tukacheka saaaaaaaaana. Nimefurahi sana kukutana na Rashid Abdallah Makwiru Au Chidy Benz sina mengi ya sana ya Kuongea kwani dah!
Amekuja kumpokea Shujaa huku huku studio hakutaka kusubiri.
Sallii Teknik Mau Kolimba Kiristian Kiri Paulo
#Shujaaa”

Facebook Tizneez

Instagram Tizneeez

Twitter Tizneez

Youtube Tizneez