CHIBWA KIDIGITALI NA ELEPHANT MAN

q4RxVoWh

Nishai ni wimbo wake uliompa tuzo ya KTMA mwaka 2014 katika kipengele cha ragger dance, ambapo wimbo huo alimshirikisha mkali Juru, na upande wa production ulifanyika na mkali Mesen Selecta.

Chibwa ambae amekuwa kimya kwa muda mrefu sasa, mapema leo Chibwa amesema “Kweli nipo kimya kwa muda mrefu ila ujio wangu ninaokuja nao sasa utaonyesha ni kiasi gani nilikuwa najipanga. Ujio wangu ni tarehe 22 mwezi huu na mzigo huu nimefanya na Elephant Man na ngoma inaitwa Digital. Itaanza audio halafu baadae itafuata video. Ila ujio huu utakuwa katika utofauti mkubwa na kazi nyingine ambazo umewahi kusikia kutoka kwangu. Pia kwasasa nina menejementi nzuri ambayo inasimamia kazi zangu vyema.”

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez

 

 

 

 

Source Ladha 3600 Efm