Boshoo kinara wa mtaa mwenye kanda mseto mkononi

Boshoo kinara wa mtaa mwenye kanda mseto mkononi.

Hakuna mtaa wenye mapendo na hiphop na wasijue Boshoo ni nani. Ingawa sasa tumeona hata wale ambao ni wasikilizaji wazuri wa Radio kujua uwezo wa Boshoo.

Sisi Tizneez tulimfahamu Boshoo mwaka 2015 na tuliweza kufanya nae mahojiano juu ya kanda mseto yake ambayo ni Ujamaa shari.

Ambapo wapo wasanii wakubwa na tunawaona bora ila hawana kanda mseto, kiukweli ni aibu.Hivyo yapasa hawa wenye bidhaa mkononi wapewe nafasi njema.

Kanda mseto hii ya Ujamaa Shari imefanyika katika mikono ya Ngwesa,na inapatikana katika mitandao ya kijamii.

Lakini pia kwa wale ambao mmekuwa mkiuliza zaidi yakuwa ni kwa namna ipi tutapata kazi za Boshoo unaweza kumcheki hapa 0718 84 44 62.

Kanda Mseto ya Ujamaa Shari ina nyimbo 10, ambapo ni

1.tafakari ft gettho ambassador

2.Tanga boy

3.Bitch love ft jeff duma

4.maisha yangu

5.walete ft dizasta

6.ujamaa shari ft malle

7.buzi la matozi

8.mziki ft bokonya

9.utunzi ft bokonya

10.kwa ajili yako

Tizneez tulishajipatia nakala yetu tangu 2015, hivyo na wewe ni vyema ununue kazi yake, tuache kusifiana tu wewe mkali wakati haununui kazi ya msanii husika.

#TuzungumzeMuziki