BONTA AZUSHIWA KIFO,ASEMA AMESIKITISHWA NA UVUMI HUO

bonta

Msanii aneyeunda kundi la Weusi Bonta Maarifa ambae pia amewahi kufanya vizuri na ngoma kama,leta baadae,hip hop na nauza kura yangu na nyingine nyingi.

Baada ya uvumi kutapaka katika mtandao wa kijamii facebook kuhusu kifo cha mwana hip hop Bonta,Team tizneez ilimtafuta msemaji wa Weusi Nikki wa pili kutaka kufahamu ukweli wa tukio hilo,akiongea kwa njia ya simu msanii Nikki wa pili alisema”hakuna kitu kama hicho,subiri niongee na harafu nitarudi kwako.

Baada ya muda mfupi Nikki wa pili aliitafuta Team tizneez na kutoa na namba ya Bonta ili tuweze kuongea nae na kupata ushahidi kamali kutoka kwa mhusika mkuu ambaye ni Bonta.

Bonta akiongea kwa njia ya simu  alisema”tuache hizo habari sio za kweli na muda huu nipo kwa joh makin hapa kwake,hivyo naomba watu wajue mimi ni mzima na nipo na mambo yangu.

Untitled

Unaweza kuwa rafiki yetu faceboo.com/tizniz

instagram.com/tizneez

twitter.com/teamtizneez