Bob Junior Aja na mipango tofauti

Bob-Jr

Bob Junior Aja na mipango tofauti

Ni mwaka sasa tangu mtayarishaji na mwimbaji muziki wa kizazi kipya Bob Junior tokea Sharobaro Records kuwa kimya katika uwanja wa bongo fleva.

Mapema leo hakusita kuweka sababu za yeye kuwa kimya ambapo amesema “Nilikuwa kimya nikijaribu kuja kwa muziki mwingine sio kusikika vile nilivyozoeleka. Lakini pia ujio wangu huu niliofanya na Chamelone sio tu utaishia hapa bali ni maandalizi ya album yangu ambayo itatoka mwisho wa mwaka huu.

Katika mauzo tayari nimeshazungumza na makampuni kadhaa hivyo nikitimiza masharti yao basi wao ndiyo watakaosimamia album hiyo. Album nafanya kutengeneza heshima yangu hata baada ya kuacha muziki au kutoweka katika uso wa dunia. Ni aibu msanii una miaka 6 mpaka 7 kwenye muziki na una album mmoja.

Na katika album hii utasikia kolabo za wasanii wengi ambao wengi hukuwategemea.

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez