Billnas Ni msanii hewa?

hqdefault

Billnas Msanii hewa?

Hewa ni wimbo wa Truebadour ambao ndani yake alizungumza mengi kuhusu muziki wa kizazi kipya, kuanzia ngazi ya wasanii, watangazaji mpaka wadau.

Wimbo wa hewa unamgusa Billnas moja kwa moja katika upande wa kufanya show, ni wazi inaonyesha Billnas ni msanii hewa kwenye jukwaa.

Raha ni wimbo wake uliomtambulisha katika ramani ya muziki wa kizazi kipya, ambapo katika wimbo huo aliweza kumshirikisha Nazizi kutoka Kenya.

Ligi ndogo ilifuata kabla ya wimbo wake unaofanya vyema sasa Chafu Pozi, ambao umeweze kushika chati mbalimbali za radio na runinga.

Katika uzinduzi wa show ya Fiesta Mwanza Billnas ni moja ya wasanii ambao walipata muda mzuri wa kushambulia jukwaa hilo mbele ya mashabiki wengi waliojitokeza.

Kiuhalisia Billnas amefanya show ambayo ipo chini ya kiwango, show yake ilikuwa na kasoro nyingi. Nadhani labda alipania zaidi kimwili na sio kiakili, unapopania kufanya jambo zuri lazima uandae akili sio mwili. Mwili ni kitu cha mwisho maana mtaji ni akili.

Show ya Bilnas ilikuwa ni kelele za hali ya juu, kuanzia yeye mwenyewe mpaka back up vocal wake ambaye alionekana kupayuka kama mtu ambaye hakuwa anajua kilichompeleka pale jukwaani.

Billnas hana wa kumlaumu zaid ya nafsi yake, sitaki kuamini kama dunia ya leo anashindwa hata kutazama show mbalimbali dunia ili kuweza hata kujifunza jinsi ya ufanyaji show.

Waswahili husema “Ukipewa nafasi itumie” Hivyo nafasi ambayo umepewa na kamati ya Fiesta ni vyema kuitumia vyema.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube Tizneez