BEN POL AELEZEA KIUNDANI MOJA MOJA

bens
Nikikupata,pete,samboira,unanichora hizi ni baadhi ya nyimbo za mkali Ben Pol ambazo zimewahi kufanya vizuri katika muziki hapa Tanzania na nje pia.
Ben pol ambaye kwasasa anafanya vyema na wimbo wake wa Sophia upande wa audio na video ambapo umeweza kuingia katika chat mbalimbali za vituo tofauti vya radio na television.
Baada ya siku kadhaa kupita tangu aachie wimbo wake wa moja moja alifanya Na Thabby Lee,Team tizneez ilimtafuta kujua mipango zaidi
Akiongea kwa njia ya simu Ben Pol alisema “Moja moja ni bonus track tu ambayo nimetoa kama zawadi kwa mashabiki wangu ila naweza pia nikaufanyia video,lakini sio official realese ila official song inakuja baada ya mwezi mmoja,ingawa bado sijajua itoke nyimbo gani maana nimefanya nyimbo nyingi.Ila mashabiki wangu siwezi kuwaangusha nina kazi nzuri hivyo wakati ukifika kila kitu kitakuwa sawa.
Mwisho.
Unaweza kuwa rafiki yetu facebook.com/tizniz

instagram.com/tizneez

twitter.com/tizneez