BEN PAUL YUPO KINYUME NA KAULI ZA WASANII NA WADAU

Ben-Paul

BEN PAUL YUPO KINYUME NA KAULI ZA WASANII NA WADAU

Katika kile kinachoendelea kutoka kwa wasanii walio wengi, wadau, pamoja hata na watangazaji, ambao wengi wao wameendelea kuwaaminisha wasanii walio wengi kuwa album haina faida hata kudiliki kusema haiuzi kabisa.

Mapema wiki kadhaa zilizopita team tizneez aliandika makala hii “Wasanii wengi wa bongo bado chipukizi kwa kukosa album” ni wazi wengi wamekuwa na majina makubwa hata kutoa nyimbo nyingi tangu kuibuka kwao lakini ni wazi wana mfanano wa msanii chipukizi.

Ben Paul hakusita kuweka wazi mtazamo wa kuachia album hivi karibuni, na hii itakuwa ni album yake ya pili wakati wengine wakiendelea kusuasua na kusikiliza mawazo ya watu Ben Paul anazidi kutengeneza biography yake vyema.

Lakini kweli album haziuzi? Mbona wasanii wa dini, taarabu na hata bolingo wameendela kuuza kila iitwapo leo?

Album ya Ben Paul itakuwa na nyimbo 12 na mpaka sasa bado hajaipa jina album hiyo licha ya kusema utasikia sauti kama ya Mwana Fa, Nameless, na wengine wengi katika album hiyo.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez