BEN PAUL NI KUTAFUTA KICK AU AMETUMWA KWA ALLY KIBA?

Ben-Paul1

Nikikupata ni wimbo ulitambulisha msanii Ben paul katika ulimwengu wa bongo fleva.Ben paul ambaye watu wengi wamezoea kumuoana akiwa katika sura ya upole lakini ni mkali katika swala zima la uimbaji wa rnb.Ukali wake amethibitisha katika nyimbo kama.Pete,Maneno Maneno,Sophia,Jikubali,Samboira,unanichora na nyingine nyingi.

Ni masaa machache kama sio siku tangu kuwepo na vita ya kutupiana maneno katika mitandao ya kijamii hususani mtandao wa picha Instagram,baina ya mashabiki wa Ben paul na Team kiba.Hii imeanza pale tu baada ya msanii Ben Paul kuandika katika mtandao wa twitter kuhusu Ally kiba ambapo ameandika”Bro @officiaalikiba me naona kama unakuwa overrated harafu inakugharimu au hakigharimu?”

Na baadae kupitia mtandao huo huo wa twitter msanii nguli Ally Kiba nae hakusita kujibu,Ambapo aliandika”Inshaallah kheri @iambenpol asante kwa kunyoosha kidole sio makosa yako ni dua inafanya kazi yake#kingkiba”

Baada ya hapo swala hili likachukua sura nyingine ambayo imekuja na maswali mawili.je Ben Paul anatafuta kick?au Je Ben Paul ametumwa?.Haya ni maswali ya walio wengi sasa,lakini licha kuuliza hayo yote pia jaribu kufikiri je kama ametumwa ametumwa na nani na kwasababu gani?.Lakini pia ikumbukwe Ben Paul sio msanii wakuwa tofauti yani (Bifu) na wasanii wengine au msanii mwenzake.

Shetani gani amemkuta Ben paul au watu wameshindwa kumuelewa nini amemaanisha?Kwa mitazamo ya wadau wa muziki imetafiriwa tofauti zaidi kuliko wale mashabiki walio wengi wanaendelea kumtukana msanii Ben paul.Kabla ya wimbo wake mpya aliyaofanya na msanii toka Kenya Avril mara ya mwisho alitoa Sophia,Lakini Sophia haukufanya vizuri kama watu wengi walivyo mzoea Ben paul.Sasa anatarajia kutoa video yake mpya ya wimbo aliofanya na Avril kwaiyo niwazi Ben Paul anatafuta kick zaidi na kama ni kick je aliwaza juu ya wingi wa mashabiki wa Ally kiba(teamkiba)?

Game ya muziki wa bongo fleva imekuwa na mabadiliko yaliyo mengi.Fid q alisema”media zinapromote bifu wanadai zina kuza mziki”Hii imeonekana wazi leo baada ya Ben paul kupata interview nyingi.Mpaka sasa imeshakuwa tofauti kubwa kati ya team kiba na Ben Paul,lakini sio Ally kiba na Ben Paul maana Ally Kiba mpaka sasa hakuna kibaya alichosema zaidi ya mashabiki wake kuendelea kumshambulia kwa matusi msanii Ben Paul.

Swala la kutumwa limekuwa likisemwa pia na hapa amekuwa akitajwa Diamond Platnumz.Lakini tusiwe watoa hukumu zaidi na kuhisi watu kama wamefanya vitu flani ili tufurahishe mioyo yetu.Kikubwa cha kujiuliza kabla hata hujasema usichokuwa na uhakika nacho jiulize swali dogo tu Diamond Platnumz amtume Ben Paul ili iweje?na yeye imsaidie nini katika muziki wake?.Nafikiri tena kwa level aliyokuwa nayo Diamond na uongozi wake wanawaza zaidi kwenda mbali zaidi ya pale sio tena kuanza kurumbana na kupotezeana heshima.

Kuandika aliyoandika Ben Paul ni maamuzi yake haipo katika imani ya kutumwa.Nadhani kutumwa angetafakari zaidi ya juu ya kuchafua cv yake katika mziki huu wa bongo fleva kutokuwa na bifu tangu anaanza mziki wake.

“kabla ya kusema mdomoni kitafakari kichwani kina maana kwa jamii iliyonizunguka?mapokeo yake je yatakuaje?”

Bifu sio kitu kizuri katika mziki,siamini katika bifu ndo mziki unakuwa bali naamini katika bifu mziki unashuka.Tunakosa radha nyingi baina ya wasanii kwa wasanii kushindwa kufanya kazi shauri ya bifu.

Let’s support our Bongo fleva.

Powered by tizneez.com

Twitter@tizneez

Instagram @tizneez

Facebook@tizneez