Ben Paul Ajitenga na wasanii magumashi

hqdefault

Ben Paul Ajitenga na wasanii magumashi

Wimbi la wasanii wakubwa wenye mfanano na wasanii chipukizi kwa kukosa album limeendelea kukua kila leo. Ni wazi wapo wasanii wakubwa ambao mpaka sasa wamefikisha miaka hata 6 kwenye muziki na hawana album.

Ben Paul hakusita kuweka mtazamo wake juu ya kutoa album ambapo ameeleza “Mwaka huu nakwenda kutoa album, na album itakuwa na wakali tofauti. Sijali changamoto za album ila mimi sio msanii magumashi. Hata kama ikitokea msanii mwingine amekuja kutoka nje akiuliza kuhusu album niweze kuzungumza”

Ben Paul kwasasa anafanya vyema na wimbo wake wa moyo mashine, ambao ni wazi umeweza kupenya mpaka kwenye vituo vikubwa vya runinga katika baadhi ya nchi za Africa.

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez