Belle 9 Nae ahoji Darassa yuko wapi?

Belle 9 Nae ahoji Darassa yuko wapi?

Kupitia mtandao wa Twitter kwenye ukurasa wake msanii Belle 9 ameandika “Darasa yupo wapi jamani?

Na hakika hisia za wengi ni yakuwa amekuwa katika dimbwi la matumizi ya dawa za kulevya.

Na Team tizneez tumeendelea kumtafuta bila mafanikio maana si mtu ambaye anapokea simu wala kujibu barua pepe.

Ni wazi tukisikiliza Sikati tamaa, haki sawa, tunaishi, weka ngoma,mikono juu, kama utanipenda, too much, muziki, na hasara roho kwa hakika huu muziki bado unamuhitaji vyema Darasa.

Tuna kila sababu ya kuuliza Darasa yu wapi?
Na hakuna jambo analopaswa kuficha hata kanakwamba ana tatizo au maradhi.

Maana mswahili hunena yakuwa “Mficha maradhi kifo humuumbua”

Lakini katika kweli huenda akawa ni mwenye fedheha ya kuona aibu mbele ya jamii na mashabiki zake juu ya tatizo lolote lile.(Kushuka kimuziki au Matumizi ya dawa za kulevya)

Ila katika kweli yenye kweli anapaswa “Kuidharau aibu” ili aweze kujikomboa vyema.

Bila kuidharau aibu hakika atabaki katika shimo baya ambalo katika uhalisi ni baya zaidi.

#TuzungumzeMuziki