Belle 9 “Kwa kizazi hiki hakuna wakuchana kama Nikki Mbishi

Belle 9 “Kwa kizazi hiki hakuna wakuchana kama Nikki Mbishi”

Sumu ya penzi, masogange, wanitaka, shauri zao, hizi ni baadhi ya nyimbo zake bora katika nyakati zote toka kwa Belle 9.

Belle 9 si msanii wa kuongea hovyo hovyo wala kuandika mengi katika mitandao ya kijamii.

Lakini leo kupitia mtando wa WhatsApp ameandika “Katika kizazi hiki hakuna wakuchana kama Nikki Mbishi”

Hii si mara ya kwanza kwa Belle 9 kuandika jambo juu ya Nikki Mbishi, maana 25.6.2017 katika mtandao wa picha aliandika “Naheshimu kipaji chake” Posti ambayo iliambatanishwa na picha ya Nikki Mbishi.

Nikki Mbishi ni moja ya wasanii wakubwa wa Hiphop na wenye uwezo wa juu. Wasanii wengi husema mengi juu yake katika kusifu uwezo ambao amebarikiwa.

#TuzungumzeMuziki