BELLE 9 ANAMALIZA MWAKA 2015 KIUTOFAUTI

Belle-ubalozi2

Belle 9 ni miongoni mwa wasanii wakali wa muziki wa rnb kutoka hapa inchini tanzania,Belle ambaye miaka yote tangu afahamike kwenye muziki amekuwa akifanya vizuri lakini mwaka huu imekuwa tofauti zaidi.

Video yake ya Shauri yao ndo video yake ya kwanza kupata air time katika vituo vikubwa barani afrika.Belle ambaye sasa anafanya kazi chini ya kampuni yake ya Vitamin Music ambayo ndiyo kampuni inayosimamia kazi zake pia za muziki.

Mapema leo hii kampuni ya Owbaz.com ilipost picha ya msanii Belle 9 na kusema,”Wellcome belle 9 as ambassador for owbaz.com this is the time to get together $ grow Tanzania”

Hii ni kwa mara ya kwanza kwa msanii belle 9 kuwa balozi wa kampuni.

Team tizneez.com inakutakia kila la kheri Belle 9.