BASATA YAFUNGIA WIMBO WA ROMA MKATOLIKI

hqdefault

Viva roma viva ni wimbo wake mkali Roma uliotoka hivi karibuni,licha ya kutoka katika muda mfupi lakini umekuwa wimbo ulipata maoni mengi kutoka kwa watu mbalimbali kutokana na mambo mengi yaliyoongelewa katika wimbo huo wa viva roma viva.

Baraza la sanaa Tanzania (BASATA), limeifungia rasmi ngoma ya Roma Mkatoliki iitwayo ‘Viva Roma’ kwa sababu hakuna ushahidi wa alichokiimba.

Taarifa ya BASATA imesema mbali na wimbo huo, pia wamezifungia nyingine zenye mahadhi kama hayo.

Ikumbukwe wiki kadhaa zilizopita, Roma aliandika Instagram kuhusu kutishiwa kufungiwa kwa ‘mkwaju’ huo.

Source Times fm