BASATA YAFUNGIA WIMBO WA NAY WA MITEGO,PIA WAMPA KALIPIO

IMG_2549

BASATA YAFUNGIA WIMBO WA NAY W AMITEGO,PIA WAMPA KALIPIO

Mapema leo Baraza la sanaa kupitia ukurasa wao wa Twitter hawakusita kuweka wazi juu ya ufungiaji wa wimbo huo wa msanii Nay wa Mitego unaoitwa Shika Adabu yako. Ambapo katika wimbo huo

amezungumza mambo mengi likiwemo la Basata “hizi taarifaz angu ziwafikie Basata,nyie ni kuku au bata msumemo usiokata kazi kufungia nyimbo mnajua shida tunazopata mgekuwa watoto ningewachapa”
Leo mapema Basata wameeamua kufungia wimbo huo rasmi Basata wamesema
“BASATA limeufungia rasmi wimbo wa ‘Shika Adabu Yako’ ulioimbwa na Msanii Nay wa Mitego kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili,uchochezi.
BASATA litampa karipio kali Msanii huyo na kumwagiza kuacha kuutangaza wimbo huo kkt media vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa.
kifungu cha 4(1)(j) & 4(2) cha sheria ya BASATA kinalipa Baraza mamlaka ya kuratibu/kufuatilia mienendo ya mtu yeyote anayehusika na Sanaa.
Vifungu hivyo,vinalipa nguvu Baraza kulinda maadili ya kitaifa na kufanya jambo lolote lile katika Sanaa kwa faida na ustawi wa taifa.
BASATA halitavumilia hawa ‘wasanii’ wachache wanaotaka kuigeuza tasnia ya Sanaa na wasanii genge la wahuni,wasio na staha,wa kudharaulik
Wasanii wengi wanafanya kazi zao vizuri,kwa kubuni kazi zenye ubora na zinazolipa sifa taifa,wachache wanaharibu.Wanapakaa matope.
BASATA limekuwa likipokea simu za maswali na malalamiko kutoka kwa waandishi wa habari na wadau wa Sanaa kuhusu wimbo huo.Ni wazi haufai”
www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez
Instagram tizneez
Youtube tizneez