BASATA MKO NYUMA YA MUDA,KUNA MENGI YA KUFANYA SIO KUFUNGIA NYIMBO

images

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ni taasisi ya umma lililoundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 23 ya Mwaka 1984.Historia inaonyesha kuwa, Sheria ya kuunda upya Baraza hili ilifanywa kwa kuunganishwa Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa ya Mwaka 1974 na Baraza la Muziki la Taifa (BAMUTA) ya Mwaka 1974. Baraza liliundwa ili lisimamie maendeleo ya sanaa nchini

Baraza la Sanaa Tanzania liliundwa kwa malengo mengi mazuri,lakini lilitengenezwa kwa mujibu wa Sheria Na. 23 ya mwaka 1984, Majukumu ya Baraza ni kama, Kufufua na kuhimiza maendeleo ya kazi za Sanaa, Kufanya tafiti wa masuala mbalimbali ya sanaa, Kutoa ushauri na misaada ya kitaalamu kwa asasi au watu wanaojihusisha na shughuli za sanaa, Kuratibu shughuli za sanaa zinazofanywa na watu au taasisi mbalimbali, Kutoa na kuimarisha mipango ya mafunzo kwa wadau wa sanaa, Kuishauri Serikali juu ya mambo yahusuyo maendeleo na uzalishaji wa kazi za sanaa. Kuhamasisha maendeleo ya sanaa kwa njia ya maonyesho, mashindano, matamasha, warsha na semina., Kuanzisha, kukusanya na kuhifadhi ikiwa pamoja na zile zinazohusu watu, asasi, taasisi, vifaa na miundo mbinu inazohusiana na sanaa, Kusajili wasanii na wale wote wanaojihusisha na shughuli za sanaa.

Si mara ya kwanza kusikia Basata wamefungia wimbo au kumfungia msanii kwa kufanya vitendo viovu au kuimba nyimbo zenye lugha mbaya katika majukwaa mbalimbali wanayokuwepo.Na msemaji wa Basata husema au huweka wazi sababu zilizofanya wafungie wimbo au kumfungia msanii.Ndani ya mwaka huu tulishuhudia msanii Shilole akifungiwa kwa kosa la utovu wa nidhamu akiwa kwenye jukwaa wakati akifanya show yake huko nchini Belgium ambapo alionekana akiacha eneo kubwa la mwili wake wakati akiwa kwenye jukwaa. Basata hakusita kukumea kwa ukali jambo hilo ambalo lilionekana wazi ni jambo baya kwenye sanaa.Na adhabu yake ikawa ni kutojihusisha kazi za sanaa ka muda wa mwaka mmoja asishiriki katika matamasha lakini tumeona leo yupo katika majukwaa ya siasa na akiwa na kama mtumbuizaji je hii maana yake nini?au mpo kisiasa au sio wao wanahusika?

Tuyaache ngoja nirudi kwenye lengo ila hayo ni maswali ambayo wanayo watu wengi zaidi ninaokutananao kila siku wenye kupenda sanaa

.Afande sele aliwahi kusema”huu mziki una hela zaidi ya hizi tunazopata kama basata wataamua kusimamia sanaa vilivyo hakika nchi itafika mbali kupitia sanaa”

Nash Mc ni moja kati ya wasanii waliowahi kukumbwa na kimbunga cha kufungiwa wimbo wake wa kaka suma iliyotoka mwaka 2013 na kufungiwa wiki kadhaa mbele.Na muda unaofungiwa wimbo huo wa kaka suma tayari ulishazagaa kila kona za mitandao ya kijamii licha ya kuchezwa mara nyingi katika vituo vya radio ndani na nje ya nchi.Nash mc alisema “Sijastuka wimbo wangu kufungiwa ila nimeshangaa ukweli unanyimwa nafasi lakini ujumbe wangu umefika kwa wahusika naamini nilichokisema kuhusu wananchi kitafanyiwa kazi”wimbo wa kaka suma ni wimbo uliotoka maalum kipindi cha kupanda kwa nauli katika vyombo vya usafirishaji.Na moja ya mistari iliyofanya wimbo huo kufungiwa ni “nikisema niandamane nitaandamana na mabomu anaeniongoza amelala kule dom,uliza uteke jifanye mdai haki rumande usekwe mabwempande wakupeleke,tuduimishe amani amani ina faida gani,mabomu ya machozi na magari ya kuwashawasha ipo siku yatafyata,wonyonge wakichoka wanageuka wahasi”

Mapema mwaka huu tumesikia tena wimbo wa msanii Roma Mkatoliki viva roma viva nao umefungiwa. Baraza la sanaa Tanzania (BASATA), “limeifungia rasmi wimbo wa Roma Mkatoliki uitwao ‘Viva Roma’ kwa sababu hakuna ushahidi wa alichokiimba.Taarifa ya BASATA imesema mbali na wimbo huo, pia wamezifungia nyingine zenye mahadhi kama hayo.

Wimbo viva roma roma ni wimbo uliotoka miezi kadhaa nyuma, na kupitia tovuti ya mkito imeonyesha wazi kuwa ni wimbo ulipakuliwa mara nyingi zaidi kwenye tovuti hiyo ambayo ndio tovuti pekee yenye dhamana ya kuweka wimbo wa msanii Roma Mkatoliki.

Muda mchache baada ya Basata kufungia wimbo wa Roma aliandikia kupitia mtandao wa picha (instagram) Life is not fair tunakufa masikini kwa kuwatete wanyanganyi eeh mungu baba wa mbinguni nisaiidie #politics #justice #freedom #vivaromaviva

Sasa swali ni je unadhani kufungia wimbo muda huu unasaidia nini? Kwa maana tayari inaonyesha wazi tayari watu wengi wameshaupata kupitia mitandao,je hamuoni kama mpo nyuma ya muda? Maana kitendo cha kuchezwa wiki mbili katika radio station inamaana tayari imeshapata wasikilizaji wengi

Kuna haja ya kufanya maboresho mengi katika kazi zenu za kila siku ili tufikishe sanaa yetu ya Tanzania mbali zaidi ya hapa tulipo.

Ila kwasasa mpo nyuma ya muda kuna mengi ya kufanya sio kufungia nyimbo.Mungu ibariki sanaa yetu.

Unaweza kuw rafiki yangu

Facebook.com/tizniz

Twitter.com/tizneez

Instagram/ tizneez