Barua ya wazi kwa Dj Fetty

Barua ya wazi kwa Dj Fetty

Nimeona kila mtu amesahau kuhusu huyu dada ambaye ni mtangazaji mstaafu kutoka radio ya watu Clouds Fm. Aliyeondoka na uwezo wake mkubwa na mpaka leo pengo lake bado lipo.

Pia nirudi kwenu Tizneez.com wakati wote mnaandika mambo mazuri juu ya bongo fleva na hiphop na kiukweli mnaandika vizuri sana licha ya kuonekana mnaboa maana wengi hawana upeo wa kuchambua kile mlichoandika kwa kuwa tu mnatumia sana misemo ya wahenga . Wengi wapo kwa kuripoti lakini nyie mpo katika mlengo wa uchambuzi na niwapongeze kwa hilo.

Nimefuatilia sana Makala zenu ambazo zilimuhusu zila lakini wasanii wengine na hata yale yahusuyo muziki wote kwa ujumla.

Wapo ambao wameona kuwa ni kama mnamkandamiza Zilla ila hapana mlioandika kama Zilla angesoma ni wazi angekuwa katika mahala salama na angejua cha kufanya. Ila kwa hasira zake hakusoma na niliona pia alivyokua anaandika juu ya yenu kawashutumu kama mnamuongelea vibaya. Nawapongeza kwa uelewa wa kutokujibu vibaya juu yake bali kubaki katika misimamo yenu na Makala bora wakati wote.

Lengo la kuandika barua hii ni kawakumbusha nyie kwanza kuwa Dj fetty ni mtu ambaye mlipaswa kumtafuta kuzungumzia swala la zila. Lakini na nyie hua nawaona kama ni watu ambao hamtoi nafasi kwa mambo mengi ambayo yanahusu Clouds.

Hili halina kificho mara tu baada ya Dj fetty kuandoka Clouds ni wazi nguvu ya zilla ilishuka na Billnas kupanda. Sina hakika wala sijui kama mnajua hilo, lakini lengo langu kuu ni kutaka Dj Fetty amtafute Zilla na kuzungumza nae kuwa shida ni nini hasa mbona haeleweki?

Naamini kabisa Zilla hana cha kuficha juu ya Dj Fetty maana hata katika wimbo wake kwa kwanza alisema “Fettie ndio kaniintroduce kwenye game” hivyo kwa ukaribu huu anaweza kusema yale ambayo yanaonekana hayapo sawa kwa Zilla.

Nichukue nafasi kumwambia dada Fetty najua hayupo katika maswala ya Radio tena ila naamina ana nguvu ya ushawishi juu ya zilla kuwa sawa na sio alivyo sasa. Mimi ni shabiki mzuri wa Zilla na naamini kabisa msaada juu ya Zilla upo kwa Dj fetty sio kwa watu wengi ambao huandika mitandaoni tu kuwa zilla hayuko sawa, sasa kama hayuko sawa wao wanamsaidia nini?au ndo ilimradi waonekane tu.

Naamini zilla anahitaji kuongea na mtu kwa kina zaidi sio maneno ya mtandaoni tu kama wengi wanavyoandika. Tusisubiri mpaka kipaji hiki kipotee ndio tuanze kusema ooh tatizo lilikuwa hivi muda huu ni muda wa kukaa nae kitako na kuzungumza nae.

Tafadhari dada fetty mtafute zilla zungumza nae na sio mpaka tujue maana hatujui maisha yako sasa ila fanya kusaidia tumuone zilla akiwa sawa tumechoka na porojo za mtandao na maneno ya wengi kuwa zila hayupo sawa.

Narudia tena naomba dada utoe neno juu ya zilla najua jinsi zilla anavyokuheshimu najua kila kitu kitakuwa sawa sana.

Najua Tizneez ni watu makini haitakuwa ngumu kwa nyie kuposti hii barua yangu najua nguvu yenu ndogo mnavyoiitumia vizuri.

Mbarikiwe na msiache Makala mnazoandika mungu awabariki Mungu mbariki King Zizi

 

Nakumbusha dada fetty usisahau na zingatia swala hili plz plz plz

Natanguliza Shukrani zangu kwako.

Mimi shabiki tu ambaye sijataka tu jina langu liwe wazi maana hawakawi kusema natafuta kiki. Asanteni Tizneez.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa