Barnaba Na mawazo ya Joh Makini na Mwana Fa.

b5e1Barnaba-800x533-2

Barnaba Na mawazo ya Joh Makini na Mwana Fa.

High Table Sound ni studio inayomilikiwa na msanii Barnaba ambaye ni miongoni mwa wasanii bora wa kiume katika upande wa bongo fleva.

Barnaba ametambulisha vijana wake wawili ambao ni Mula pamoja na Ice boy. Ambapo wamekuja na ujio unaoitwa Tumbua Majipu..

Barnaba hakusita kuweka wazi kuhusu kusaini wasanii wa hiphop wakati wengi wao wanaamini hiphop sio muziki wa biashara katika ramani ya muziki wa kizazi kipya. Barnaba alisema “Muziki ni inspiration kama muziki utafanywa kwa njia nzuri basi utakuwa biashara. Kila kitu kinahitaji ubunifu wa hali ya juu hivyo vijana wangu nikiwatazama naona kabisa wakina Joih Makini na Mwana Fa wapya.”

Ni wazi ana mawazo mapana juu ya msanii kama Joh Makini na Mwana Fa lakini ni vyema kuwaza tofouti ili kutoa swala zima la kuigana ambalo pia limekuwa ni kero katika muziki wa kizazi kipya. Maana ni wazi wasanii wengi wamekosa kuwa na utambulisho sahihi wa kazi zao. Hivyo hupelekea kushindwa kufanya vyema katika muziki huu wa kizazi kipya.

Team tizneez inaamini katika kipaji chaka Barnaba hivyo hatutegemi kuona ukimtengeneza Joh Makini mwingine au Mwana Fa bali wasanii wapya wasiofanana ni mtu yoyote.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez