Barnaba Na hoja dhaifu mbele ya wakongwe wa muziki kizazi kipya.

Barnaba

Barnaba Na hoja dhaifu mbele ya wakongwe wa muziki kizazi kipya.

Malalamiko makubwa ya wakongwe wengi wa muziki ni kunyimwa air time katika vituo mbalimbali vya radio na runinga. Ila sasa si kwenye vituo vya radio na runinga tu bali hata katika blogs.

Kimsingi wanayo hoja yenye maana juu ya upendeleo ulipo sasa. Wapo ambao wenye mawazo madogo kusema muziki wa sasa umekuwa mgumu hivyo ni ngumu wasanii wakongwe kufanya vyema. Kiukweli jambo hili halina uhalisia na sasa, maana muziki wa zamani ndio ulikuwa mgumu kuanzia ngazi ya studio mpaka kwenye vituo vichache mno vya radio na runinga. Ila tuliweza kusikia wasanii wengi wazuri ambao wametoa kazi zenye kuishi mpaka leo.

Muziki wa sasa umekuwa mgumu katika ngazi ya upendeleo Nash Mc aliwahi kusema katika wimbo wake wa “Mwanangu” “Kuna washikaji ambao wanatoa hela wapigiwe nyimbo zao hata kama wanambwela, chana unavyoweza imba mpaka upasuke kama hujatuma vocha ndoto za kuwa nyota na kutoka zifute, hewani siku moja nyingine kapuni. Ukipeleka wimbo utaulizwa unatoka mkoa gani? Kama ni bongo fleva utaulizwa unatoka nyumba gani?”

Niliwahi kuzungumza na Mchiz Mox ambapo alisema “Wasanii wa zamani sio kama hawafanyi vyema ila wengi hatupendi habari za kuhonga mtangazaji wala Dj au kutumia njia ambazo sio sahihi ilimradi usikike hewani”.

Hivyo katika hayo ni wazi wasani wengi wa sasa hutumia njia ambazo sio sahihi ilimradi wasikike zaidi hewani. Kwa msanii Barnaba kusema “ni ngumu kwa wasanii wa kitambo kupata ‘air time’ sasa, kwani wasanii wachanga nao wanafanya vizuri pia katika uhalisia ni hoja dhaifu mbele ya watu wanajua muziki na wachambuzi makini.

Kimsingi ni wazi hakuna usawa katika vituo vingi vya radio na runinga, bali sasa kumekuwa na ushikaji, ukanda, na bosi kasema ndivyo hufanya wasanii wengi wakongwe wasipate nafasi lakini si kama eti wasanii wa sasa wanafanya vizuri zaidi.

Ni vyema kujenga usawa na tukapata kupata muziki mzuri radio na kwenye runinga maana wengi husema “Radioni na Runinga hakuna muziki mzuri”

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez