BARAKA DA PRINCE AELEZA SABABU ZA KUTOFANYA VIDEO YA WIMBO NA RUBY

Baraka

Nivumilie ni wimbo wake Baraka aliyomshirikisha Ruby ambapo ulikuwa wimbo bora katika website ya tizneez hasa pale tulipoamua kuweka nyimbo 10 bora za mwaka 2015.Baraka alipata kushika nafassi ya 7 katika nyimbo hizo 10 zilizofanya vizuri 2015.

Kama ilivyozoeleka sasa wimbo wowote unaofanya vizuri basi pia hufuatiwa na video nzuri,lakini imekuwa tofauti kwa msanii Baraka

Baraka hakusita kuweka wazi sababu zilizofanya video hiyo ya nivumilie isitoke, Ambapo alisema”Kwanza kabisa nivumile nilifanya katika uongozi wangu wa kwanza,hivyo ni wazi wimbo huu ulihusu zaidi uongozi wangu ule wa kwanza.Hivyo uongozi wangu mpya tuliamua kuachana na wimbo huo tulitaka tufuatilie lakini nikaona utatusumbua.Tukaona tuache tufanye kazi maana hakika ingechukua muda mrefu, lakini hata hii kazi yangu mpya ni nzuri hivyo mashabiki wangu waendelee kunipa ushirikiano.

www.tizneez.com

twitter tizneez

instagram tizneez

facebook tizneez

 

Source Fnl Eatv