Baraka Da Prince Adai anaongoza kwa kusingiziwa

1453375335_9920_b

Baraka Da Prince Adai anaongoza kwa kusingiziwa

Siwezi ni wimbo wake unaofanya vyema katika vituo mbalimbali vya radio na runinga ndani na nje ya nchi pia. Lakini pia ni wiki moja imepita tangu atoe wimbo wake mpya aliomshirikisha Mr Blue na Ben Paul, ambapo wimbo huo unaitwa Mwambie.

Baraka alieleza hisia zake juu ya mambo mengi ambayo yanaongelewa zaidi katika mitandao ya kijamii kuhusu kuwa na mahusiano tofauti tofauti na wasichana mbalimbali. Baraka alisema “Ni wazi inawezekana kuwa msanii wa kwanza kuongoza kwa kusingiziwa matukio katika karne hii. Vitu vingi vinavyoongelewa ni vitu ambavyo vinakuwa sijui chochote na mara nyingi vinakuwa vipya kwangu.”Alisema

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez