Bajeti ya akili haijatumika kwenye video ya Belle 9.

belle-9-nakupenda

Bajeti ya akili haijatumika kwenye video ya Belle 9.

Ni ukweli usiopingika wengi walikuwa wakisubiri kwa hamu video ya Burger Movie selfie remix ya mkali Belle 9, ambayo ndani yake amewashirikisha Izzo Biznes, Mr blue, Maua Sama, Gnako, na Jux.

Ni uwazi usiopingika video ya kwanza ya wimbo huu ulistua walio wengi maana video ikuwa kubwa ambayo licha ya bajeti ndogo ya pesa ila ni wazi bajeti kubwa ilikuwa kwenye akili. Ni kawaida siku hizi wengi wakipanga bajeti ya video hukimbilia kukodisha magari,boti,maeneo lakini wengi wao husahau bajeti ya akili katika kufanya kazi hiyo.

Ni jana usiku video ya Burger Movie Selfie Remix ilitambulishwa katika vyombo kadhaa vya habari. Kiukweli ni video mbaya ambayo huwezi kulinganisha hata na behind the scene ya video ya kwanza. Lakini kwa mujibu wa Belle 9 amesema “Video hii imefanywa na watarishaji watatu Hanscana, Khalfan na mtayarishaji kutoka Kenya ambaye amefahamika kwa jina la Engs Click.

Lakini je hao watayarishaji watatu wamefanya kitu gani katika video hii?.Ni ukweli usiopingika ukitazama video ya kwanza ambayo alifanya mtayarishaji mmoja tu ambaye ni Gihcue ni wazi alitumia bajeti ya akili zaidi. Kuna tofauti kubwa kati ya video ya kwanza na ya sasa, hasa katika ubora wa picha hata uchanganyaji.

Wote tunajua Belle 9 yupo chini menejimenti sasa, ila siamini katika menejimenti yake inaonekana ni wazi ni menejimenti yenye pesa lakini sio menejimenti inayojua soko la muziki linataka kitu gani. Ukitazama menejimenti yake ipo kumsaidia kipesa na sio mawazo, ubunifu ambayo yatamsaidia Belle 9 kusonga mbele zaidi.

Huu ni mtazamo wa Team tizneez, unaweza kuandika maoni yako hapo chini.

 

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez