Baghdad Aja na project maalumu kwa vijana

IMG-20160809-WA0004

Leo tar 10 mwezi wa 8 ninaachia rsmi wimbo wangu mpya uitwao Nipe Namba niliomshirikisha One Six ilioandaliwa na Abba Process. Lakini pia ninaizindua rasmi tour yangu ya SISHIKI BOMBA ambayo ninatazamia kuzunguka mikoa zaidi ya kumi Tanzania kutoa elimu kwa wanafunzi wa ngazi ya kuanzia kidato cha nne hadi chuo kutokujihusisha na matumizi ya mdawa ya kulevya, biashara haramu na kufaya ujambazi. Tour yangu itaanzia TABORA tar 20 mwezi huu wilaya ya nzega. Hadi sasa sina msanii yoyote ambae ametokea kuniunga mkono kwenye hili lakini pindi itakapotokea nitawajuza ila yupo kijana ambae nitazunguka nae mikoa yote ambae nae kama asingeipata elimu kutoka kwangu pengine eo tungempoteza wakati ni moja kati ya wasanii wazuri sana na watakaoweza kufanya makubwa kama akipewa nafasi, nimeanza kwa kumuunga mkono wa kufanikisha amepata audio na video ambazo zote zinatoka leo kwa pamoja na audio ya Nipe Namba amemshirikisha Deddy ilioandaliwa na Duppy kwa jina anaitwa Jovie.  Hadi sasa kila kitu nafanya mwenyewe hakuna mdhamini yoyote hivyo ninawasihi sana wadau wa mziki radio station za mikoani mahoteli kuwasiliana na mimi kwa njia ya 0652 89 48 71 ili kuangalia jinsi gani tunashirikiana ili kuweza kuongeza nguvu kwenye kutoa elimu kwenye mkoa wako.

Kwa maelezo zaidi pita kwenye kurasa zangu za mitandao ya kijamii

Instagram @bagh_dad

Facebook Baghdad Pg Kweka

Email bdady2009@gmail.com