BAGDAD AWAONYA WASANII,AWEKA WAZI MTAZAMO WAKE

10482933_753130191393145_1767170172767255521_n

Wakati kampeni rasmi za uchaguzi zikitarajia kuanza hivi karibuni na tayari watu wengi wamekuwa wakisubiri kwa hamu kusikia sera za viongozi mbalimbali ambao wamejitokeza katika kugombea nafasi mbalimbali kama udiwani,ubunge na uraisi.

Wasanii wengi wamkeuwa wakipost katika mitandao ya kijamii hasa mtandao wa picha instagram na kuonyesha  hisia zao juu ya nafasi ya urais inayonekana kuwa na ushindani mkali.

Msanii Bagdad nae hakuficha hisia zake baada ya kupost katika mtandao wa instagram ambapo aliandika”Kuna position na power yani kuna nafasi na nguvu,ukijiona una nguvu usipotoshe watu wauze nafasi kama unavyotaka kuiuza wewe.Kama kweli unaamini mtu flani kafanya kazi imeonekena kausha maana kura ni siri.Hivi mnadhani wananchi hawaoni post zenu?na wananchi ni wengi kuliko nyie watu mashuhuri mnaowaambia watu wawatukanehamuogopi matusi.Ikumbukwe hizi ni kampeni na watatumia muda huutu kwani hatujifunzi tu tangu wasanii tumekuwa tukizungumzia kuhusu haki miliki je huu ni mwaka wangapi?

Ninaloliona baya ni pale wananchi wakiamua kutopiga kura huko mnapowaelekeza wapige wakapiga kwingine yatatokea kama ya tuzo fulani mwaka huu mtu akajikuta anachukua tuzo hata ya mtumbuizaji bora wakati hapigagi show.Yote hiyo ni nguvu ya wananchi to be honest napenda sana post za mtu kama djku hongera kaka hamasisha watu wasipoteze kura.Usiku mwema ndugu zangu wote wa ACT,UKAWA na CCM

Unaweza kuwa rafiki yetu faceboo.com/tizniz

instagram.com/tizneez

twitter.com/tizneez